JACK Grealish, kiungo wa Aston Villa ambaye ni nahodha wa Mbwana Samatta ameonyesha nia ya kujiunga na Klabu ya Manchester United ambayo inaelezwa kuwa wanaiwinda saini yake.
United kwa muda mrefu wamekuwa wakielezwa wapo kwenye hesabu za kupata saini ya Grealish na Jadon Sancho anayekipiga ndani ya Dortmund kwa lengo la kuboresha kikosi chao msimu ujao.
Grealish ameonyesha nia ya kujiunga na Manchester United na dau lake linatajwa kuwa ni pauni milioni 70 ambapo hivi karibuni ameonekana akibonyeza 'like' kwenye vitu vya Manchester United jambo ambalo wataalamu wa mambo wanasema ni ishara za mwanzo.
Aston Villa kwenye msimamo ipo nafasi ya 19 baada ya kucheza mechi 28 ikiwa na pointi 25 huku Grealish akiwa ni injini ndani ya klabu hiyo jambo lililowavutia Manchester United.
Post a Comment