HITIMANA Thiery, Kocha Mkuu wa Namungo amesema kuwa Clatous Chama ni miongoni mwa viungo Makini ndani ya Uwanja.
Akizungumza na Saleh Jembe, Thiery amesema kuwa kiungo huyo wa Simba ni mfano kwa wengi ambao wanajifunza kutokana na kuwa na juhudi awapo uwanjani.
"Msimu alianza kwa kusuasua ila baadaye mambo yakawa mazuri kwake ndio maana amekuwa kwenye ubora mpaka pale ligi ilipokuwa ikisimama.
"Anajituma na kufanya kile anachokipenda kwa wakati, juhudi na nidhamu ni vitu ambavyo anavyo hivyo ni miongoni mwa viungo wazuri," amesema.
Chama amefunga mabao mawili na kutoa pasi saba za mabao huku Simba ikiwa imkefunga mabao 63
Post a Comment