MUSSA Mohamed, beki wa Nkana FC amesema kuwa dili lake la kutua Yanga lipo ila Virusi vya Corona vimetibua mambo kwenda sawa.
Beki huyo, raia wa Kenya amesema kuwa hana tatizo la kucheza ndani ya Klabu ya Yanga kwani anaamini uwezo anao na akipata nafasi atafanya vizuri.
"Nimefanya mazungumzo na Yanga ila kwa sasa mambo yameshindwa kuendelea kwa kuwa kuna janga la Corona mambo mengi yamesimama mpaka pale hali itakapokuwa sawa.
"Mkataba wangu ndani ya Klabu ya Nkana unamalizika mwezi Juni hivyo ninaruhusiwa kujiunga na timu yoyote ikiwa makubaliano yatakuwa sawa nitasaini," amesema
Post a Comment