KAULI ya Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta, kuhusu kwamba hawezi kumbembeleza mchezaji kusalia ndani ya klabu hiyo kama hana nia ya kuendelea kuwa hapo, moja kwa moja inaelezwa imemlenga staa wa timu hiyo, Pierre–Emerick Aubameyang.
Kwa siku za karibuni, Aubameyang ameonekana kugoma kusaini mkataba mpya ndani ya Arsenal wakati ule wa awali ukitarajiwa kumalizika Juni, mwakani.
Wakati Aubameyang akigoma kusaini mkataba huo, amekuwa akihusishwa kutakiwa na klabu kadhaa ikiwemo Barcelona, Real Madrid na Manchester United.
“Siwezi kumshawishi mchezaji kucheza Arsenal au kujiunga na sisi, mchezaji anatakiwa kujitoa na kupambana kwa ajili ya klabu,” alisema Arteta alipoulizwa mipango yake ya usajili na namna ya juhudi zake za kuwashawishi mastaa wasiondoke klabuni hapo
Post a Comment