IBRAHIM Ajibu, kiungo mshambuliaji wa Simba amesema kuwa miongoni mwa wachezaji ambao alikuwa na muungano nao bora ndani ya uwanja ni pamoja na Obrey Chirwa anayekipiga ndani ya Azam FC pamoja na Erasto Nyoni aliye ndani ya Simba.

Ajibu alicheza na Chirwa msimu wa 2017/18 ambapo alitoa jumla ya pasi nne za mabao na katika mabao hayo matatu yalifungwa na Chirwa.

Nyoni ni beki ndani ya Simba ambayo imecheza mechi 28 na kufungwa mabao 15 msimu huu wa 2019/20 ikiwa na pointi 71 kibindoni.

Ajibu amesema:"Ni wachezaji wengi ambao ninapenda kushirikiana nao kwani ninafanya nao kazi kwa ukaribu ila miongoni mwao ni Chirwa ambaye nilikuwa naye Yanga na alifunga mabao mengi huku nami nikihusika kutengeneza pasi za mabao.

"Kuhusu Nyoni lazima uwe na beki ambaye atakupa ulinzi na uwezo wake pia wa kufunga ni muhimu hasa timu inapotafuta ushindi."

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.