GERALD Mdamu, mshambuliaji wa Mwadui FC aliyetaka kumtegua nyonga mlinda mlango wa Simba Aishi Manula, Oktoba 30, wakati Simba ikikubali kichapo cha bao 1-0 amesema kuwa anajinoa kwa kasi ili ligi ikirudi arejeshe majeshi.
Mdamu amesema kuwa kipindi hiki cha kujikinga dhidi ya Virusi vya Corona yupo makao makuu ya nchi, Dodoma huku akifanya mazoezi kwa kasi.
“Nipo zangu Dodoma kwa sasa ninachukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona na kufanya mazoezi ili kulinda kipaji changu pale ligi ikirudi nami niwe katika ubora wangu uleule,” alisema.
Mwadui FC ipo nafasi ya 12 ikiwa imecheza mechi 28 na imejikusanyia pointi 34 ikiwa imetupia 27 kimiani Mdamu amefunga mabao matano.
Post a Comment