IWAPO Yanga itakuwa siriazi kuisaka saini ya nyota wa zamani wa Klabu ya Rayon Sports ya Rwanda, Michael Sarpong ambaye atakuja kuwa mbdala wa David Molinga atatua makao makuu ya Jangwani bure kabisa.
Sababu kubwa za kumpata nyota huyo bure ni kuvunjiwa mkataba na mabosi wake wa zamani kwa kile kinacholelezwa kuwa alimsema rais wa timu hiyo kuwa hajamlipa mshahara wake kwenye kituo kimoja cha radio alipokuwa akihojiwa nchin Rwanda.
Inaelezwa kuwa Yanga ipo kwenye mpango wa kuinasa saini ya nyota huyo ambaye atakuwa na kazi ya kumchomoa kikosi cha kwanza Ditram Nchimbi na David Molinga ambao ni washambuliaji.
Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa hakuna hesabu za kufanya usajili kwa sasa kwa kuwa wakati bado haujafika.
"Mpango wa usajili wakati huu haupo ila kilichopo ni kufuatilia tu wachezaji ili wakati ukifika tusipate tabu kwa sasa hakuna masuala ya usajili," amesema.
Post a Comment