MSHAMBULIAJI wa Tottenham Hotspur, Heung-Min Son, amefanikiwa kumaliza mafunzo ya kijeshi huko kwao Korea Kusini.
Katika mafunzo hayo ya wiki tatu, mshambuliaji huyo tegemo wa Tottenham na taifa lake la Korea Kusini, amemaliza katika nafasi tano za juu kati ya watu 157.
Son alikuwa katika kambi ya jeshi la majini iliyopo Kusini mwa Kisiwa cha Jeju. Mafunzo hayo yalianza Aprili 20, mwaka huu.
Post a Comment