LUC Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa anajivunia Haruna Niyonzima, Bernard Morrison na David Molinga kwa kuwa ni miongoni mwa wachezaji wake anaoamini watakuwa msaada kwenye mechi zake zote ikiwa ni pamoja na ile dhidi ya Simba itakayopigwa Machi 8 Uwanja wa Taifa.
Siku saba zimebaki kbala ya Yanga kuikaribisha Simba Uwanja wa Taifa kwenye mchezo wa pili wa ligi ikiwa na kumbukumbu ya kulazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 Januari 4.
Akizungumza na Saleh Jembe, Eymael amesema :' Ni ngumu kuwataja wachezaji wanaojituma kwa kuwa kila mmoja anacheza kwa kujituma na wananifurahisha hasa timu inapopata ushindi. Ninapenda namna Niyonzima anavyokuwa na mpira anajua aupeleke wapi, Morrison yeye alikuwa na matatizo yake Ila nilikaa naye na sasa kila kitu kinakwenda sawa.
"Molinga yeye papara tu ndani ya Uwanja Ila akitulia sehemu moja anakupa kile unachokihitaji hasa kwa kufunga mabao, nina amini kazi itakuwa ngumu tukikutana na wapinzani wetu Simba ila tutapambana," amesema
Post a Comment