LUC Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa anaamini uwezo wa wachezaji wake unazidi kukua kila siku jambo linalomfanya aamini kwamba watafanya vizuri kwenye mechi zao zilizobakia ndani ya Ligi Kuu Bara pamoja na mashindano mengine.
Yanga jana imeshinda mbele ya Mbao FC mabao 2-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Batra uliochezwa Uwanja wa Taifa.
Eymael amesema:" Kila siku wachezaji wangu wanazidi kuimarika na kufanya kile ambacho ninakihitaji na mashabiki wanapenda kuona, kwa sasa ninaona matokeo mazuri kwa vijana wangu na hili linaleta mwanga wa kujua wapi tunakokwenda hata kwenye mchezo wetu dhidi ya Simba tutafanya vizuri,".
Mabao ya Yanga jana Machi 3 yalifungwa na David Molinga dakika ya 26 na Patrick Sibomana dakika ya 81, Machi 8 itamenyana na Simba
Post a Comment