UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa dozi waliyotoa mbele ya Singida United ni matokeo ya kujituma kwa wachezaji wake ndani ya uwanja.

Singida United ilifungua mwaka 2020 kwa kupkea kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Azam FC  kwenye mchezo wa kwanza kwa mwaka 2020 uliochezwa Januari Mosi, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Akizungumza na Saleh Jembe, Kocha Msaidizi wa Azam FC, Idd Cheche amesema kuwa wachezaji walijituma na kufanya kazi ya ziada kutafuta ushindi.

"Wachezaji walijituma na walifanya kazi ya ziada kutafuta matokeo, haikuwa kazi rahisi ila mwisho wa siku tumepata pointi tatu," amesema.

Mabao kwa upande wa Azam FC yalifungwa na Bryson Raphael dakika ya 26 na lile la pili likifungwa na Idd Seleman dakika ya 89 akimalizia pasi ya Idd Kipagwile huku lile la Singida United likifungwa na Frank Zakaria dakika ya 62.

Ushindi huo unaifanya Azam FC kuwa nafasi ya pili ikiwa na pointi 26 baada ya kucheza mechi 13 huku Singida United ikibaki nafasi ya 20 na pointi zake 7 baada ya kucheza mechi 14.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.