HENRICK Chota, mwanachama wa Yanga ambaye aligombea nafasi ya Umakamu Mwenyekiti kwenye uchaguzi wa Yanga mwaka jana, 2019 amesema kuwa miongoni mwa wachezaji anaowakubali kutoka ndani ya Klabu ya Simba ni pamoja na Clatous Chama, Deo Kanda na Meddie Kagere.
Chota amesema kuwa kabla ya Ligi Kuu Bara kusimamishwa kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona alikuwa anawafuatilia kwa ukaribu wapinzani wao ambao anaamini kuwa wana kikosi kipana na kizuri kama ilivyo kwa Yanga.
"Ninapenda uwezo wa nyota wengi wa Simba ila hawa watatu ambao ni Clatous Chama, Deo Kanda na Meddie Kagere ninawakubali.
"Simba ina kikosi kizuri kama ilivyo kwetu ila tumewazidi kwenye upande wa burudani kwani ilionekana Machi 8, kuna rafiki yangu alikuwa wa Simba alinipa tabu sana siku hiyo uwanjani," amesema.
Yanga iliwatungua Simba bao 1-0 kwenye mchezo wa mzunguko wa pili uliochezwa Uwanja wa Taifa
Post a Comment