STAA wa Manchester United, Marcus Rashford imeelezwa kuwa kwa sasa yupo fiti kwa asilimia 80 na huenda akarejea pale Premier itakaporejea mwezi ujao.


Rashford amekuwa nje ya Man United tangu Januari 16, mwaka huu, baada ya kuumia mgongo kwenye mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Wolves.

Baada ya hapo staa huyo alitupwa nje na mpaka Premier League inapigwa stop kutokana na janga la Virusi vya Corona, Rashord alikuwa nje na tayari alikuwa amekosa mechi tisa za msimu huu kwenye michuano tofauti.

 Kitendo cha Rashford kuumia kipindi kile kocha wa timu hiyo, Ole Gunnar Solskjaer alikosolewa kwa kumchezesha mchezaji huyo mechi dhidi ya Midland akijua kuwa hayuko fiti.

Pamoja na hayo, Premier kusimama ni wazi kumesaidia kumpa nafasi zaidi Rashford ya kujiweka fiti kwani kama ligi ikiendelea huenda mambo yangekuwa tofauti.


Metro imeripoti kuwa hali ya sasa ya Rashford ni nzuri na yuko fiti kwa asilimia 80 bado kidogo tu atakuwa fiti na kuendelea kupambana na wenzake.

 Rashford amekuwa akifanya mazoezi ya gym na mazoezi mengine na hii ni kuhakikisha anajiweka fiti na kuwa sawa na wenzake.Hata hivyo, United ina matumaini kuwa huenda baada ya siku 10 wakaanza kufanya mazoezi kwa pamoja huku wakizingatia ile kanuni ya kukaa mita moja.



Kwa sasa klabu hiyo inapanga kuwagawa wachezaji wake katika makundi ya watu watano kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa.

Wiki hii Jumanne, wachezaji wa United baadhi walianza mazoezi kwenye Uwanja Cheshire na walionekana wachezaji kama Paul Pogba, Victor Lindelof na Anthony Martial

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.