DAVID Molinga, mshambuliaji namba moja ndani ya Yanga amesema kuwa hana mpango wa kusepa ndani ya klabu hiyo kwa sasa.

Imekuwa ikielezwa kuwa miongoni mwa nyota ambao panga linawahusu msimu ujao ndani ya Yanga ni pamoja na Molinga mwenye mabao nane.

Molinga amesema:"Sitarajii kuondoka kwa sasa ndani ya Yanga labda wakati ujao iwapo mabosi wenyewe wataniambia niondoke ila ninachojua mimi bado ni mchezaji wa Yanga," amesema.

Yanga ipo nafasi ya tatu kibindoni ina pointi 51 baada ya kucheza mechi 27 za Ligi Kuu Bara

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.