PACHA ya mabeki wawili wazawa ndani ya Simba, Mohamed Hussein na Shomari Kapombe imejibu baada ya nyota hao kuhusika kwenye mabao tisa ya timu yao licha ya kuwa ni mabeki.
Kapombe ambaye ni beki wa kulia amehusika kwenye mabao matano huku Tshabalala akihusika kwenye mabao manne kati ya 63 yaliyofungwa.
Tshablala amefunga mabao mawili na kutoa pasi mbili za mabao ambapo pasi yake ya mwisho kabla ya ligi kusimamishwa alimpa Meddie Kagere mbele ya Singida United wakat Simba ikishinda mabao 8-0.
Kapombe naye akiwa ametoa pasi tano, pasi yake ya mwisho alimpa Kagere Uwanja wa Taifa wakati Simba ikishinda mabao 3-2.
Post a Comment