DANIEL Mgore mlinda mlango wa Biashara United anatajwa kuwekwa kwenye rada za mabosi Azam FC ambao wanahitaji saini yake jumlajumla.
Habari zinaeleza kuwa tayari mabosi hao wameanza mkakati wa kuinasa saini yake ili atue ndani ya kikosi hicho ambao ni mabingwa watetezi wa Kombe la Shirikisho baada ya Razack Abarola mlinda mlango namba moja wa timu hiyo mkataba wake kufikia ukingoni.
Februari 22 guu la kulia la Meddie Kagere lilikwama kwenye mikoni ya Mgore ambaye aliipangua penalti yake wakati Simba ikishinda kwa mabao 3-1 Uwanja wa Taifa.
Ofisa Habari wa Azam FC alisema kuwa kuna mipango mikubwa ya kuboresha kikosi ndani ya Azam FC ila kinachosubiriwa ni ripoti ya Kocha Mkuu Arstica Cioaba.
“Mpango wa kuboresha kikosi cha Azam upon a kwa upande wa kipa pia ni muhimu kwani Abarola mkataba wake unakwishwa msimu utakapoisha hivyo ni muhimu kujua itakuaje.
“Kikubwa ambacho kinasubiriwa tu kwa sasa ni ripoti ya kocha ikishatoka hiyo mambo mengine yataendelea kwani hakuna timu ambayo haina hesabu za kuimarisha kikosi,” alisema.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.