MATUMAINI yameanza kurejea kwa familia ya wanamichezo baada ya Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli, kusema kuwa kuna mpango wa kufikiria kurejesha ligi zote za Tanzania.
Tunatambua kwamba kwa mamlaka ya Serikali ina maana kwamba hatua zikifikia na kila kitu kikiwa sawa basi tutarajie kurejea kwa ligi ambazo zilikuwa zimesimama.
Tangu Machi 17 baada ya Serikali kupitia kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kusitisha masuala yote ya mikusanyiko isiyo ya lazima ikiwa ni pamoja na Ligi Kuu Tanzania Bara,Ligi Daraja la Kwanza, Ligi ya Wanawake na zile za mikoa kulikuwa na kiza kidogo.
Yote hayo ilikuwa ni hatua ya Serikali kupambana na Corona kwa vitendo kwani ni muhimu afya za wananchi zikawa salama kuliko kuendelea kucheza ilihali kuna hatari ya kupata Virusi.
Haikuwa ni Bongo pekee bali hata ulaya mambo yalikuwa hivi kwani Ligi Kuu ya England ambayo ni pendwa nayo pia ilipigwa pini kutokana na maambukizi ya Corona.
Zipo ambazo zimeshafutwa na bingwa amepatikana kwa mujibu wa kanuni zao ambapo ni pamoja na ile ya Kenya huku Gor Mahia wakiwa ni mabingwa.
Kwa hatua ambayo wameifanya inapaswa iwe somo pia kwa Shirikisho la Soka Tanzania wakati ujao kujipanga pia na kwa masuala ya dharula ili kujua mambo yanaweza kwenda namna gani.
Itakuwa ni vema kujiaandaa vizuri kwa hali zote za wakati wote ili pale linapotokea tatizo kukawa na njia ya kulitatua kwa upesi kwa kutumia kanuni.
Kwa kuwa kwa sasa kuna dalili za ligi kurudi basi itapendaeza kila mmoja akaanza kufanya maandalizi ili kujiweka sawa kwa ajili ya mapambano.
Ninaamini tayari wengi watakuwa wameanza kubadilika kwa kuchukua tahadhari na kufanya yale ambayo yanashauriwa na wataalamu wetu wa afya pamoja na Serikali kiujumla.
Wizara ya afya katika hili pia wanastahili pongezi kwani taarifa zimekuwa zikitolewa mara kwa mara jambo ambalo linaongeza umakini kwa wale ambao wanapata taarifa hizo.
Kanuni ni zilezile hazibadiliki ila kitu cha msingi hapa ni namna ya kuzifuata na kufanya kile ambacho kinaelekezwa na wataalamu wetu.
Iwapo kila mmoja akawa makini katika kufanya yale ambayo wataalamu wanaelekeza na kututaka tufanye basi itakuwa ni moja ya mbinu ambayo tumeingia nayo ndani ya vita kutafuta ushindi.
Kwa wachezaji pia ni muhimu kuendelea kuzifuata kanuni zile za afya pamoja na program ambazo mmepewa na benchi la ufundi.
Kwa wale ambao watakuwa wanazipuuzia program hizo ni wakati wao sasa kuonyesha kwamba wapo makini kwa kuanza kufanya muda huu ambao Serikali inajadili kabla ya kutoa tamko kuruhusu ligi iendelee..
Ikumbukwe kuwa vita itakuwa kali hasa baada ya ligi kurejea kutokana na kila timu kupanga kufanya vizuri kwa mechi za mwisho ambazo zimebaki.
Lala salama tunatarajia itakuwa na ushindani mkubwa ka kila timu kuonyesha kwamba ilikuwa inastahili kupata matokeo mazuri na yatakayowafikisha kwenye malengo yao.
Ninaona kabisa wakati unakuja na kila mchezaji atakuwa na sababu zake binafsi za kushindwa kuonyesha uwezo wake kisa Corona ila hilo litakuwa ni juu yake.
Jambo la kuzingatia hapa kwa sasa mamlaka husika za soka ikiwa ni TFF kuanza kuangalia ni namna gani mambo yanaweza kwenda sawa na kuanza kujipanga vizuri.
Kila mmoja atambue kwamba ni mapambano yetu wote bila kujali tajiri ama maskini ni lazima apambane ili kushinda mapambano haya.
Imani yangu ni kwamba kwenye hili janga la Corona tutapita salama na kurejea tulipokuwa awali kwenye maisha yetu na kazi zitaendelea kama kawaida ikiwa ni pamoja na kushuhudia soka safi baada ya mapumziko ya muda.
Jambo la msingi kwa sasa ni kila mmoja kuchukua tahadhari na kuamini kwamba ugonjwa upo na ligi ipo njiani kurudi maana wapo ambao walikuwa wamekata tama kuhusu kurejea kwa ligi.
Napenda kuwaomba kwamba kwa wakati huu kila mmoja awe balozi mzuri kwenye mapambano haya na tukishinda tushinde pamoja na ligi ikirudi burudani iendelee kama kawaida.
Kitu pekee ambacho kitarudisha ushindani kwenye ligi zote ni utayari na maandalizi mazuri kwa kila mmoja kabla ya ligi kuanza kuridima.
Viongozi wa Ligi Kuu Bara, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi ya Wanawake kwa yale mambo ambayo yalikuwa hayajaa sawa wakati wake ni huu sasa,
Wale wachezaji ambao bado walikuwa wamejipa likizo ni muda wa kuzinduka sasa na kuanza kujipanga upya kwa kufanya mazoezi ili kurejea kwenye utimamu wa mwili.
Viongozi ambao mlikuwa mmetoa ahadi kwa wachezaji ni muda wa kuzitimiza na kufanya yote yale ambayo mlikuwa mmewaahidi wachezaji wenu.
Kazi ya wachezaji kwa sasa ni mojs kuongeza juhudi mara dufu kutimiza zile program ambazo benchi la ufundi liliwaachia wakati ule baada ya ligi kusimama.
Pia walimu ni muda sahihi wa kupanga mpango kazi kwa ajili ya kumaliza ligi kwa mechi hizi za lala salama ambazo zimebaki kuisha.
Imani yangu ni  kwamba kila mmoja anatambua majukumu yake basi inatosha kuendelea kuchukua tahadhari pamoja na kupambana kwa juhudi pale ligi itakaporudi.
Mimi pia nimeukumbuka mpira nitafurahi kuona siku moja ligi inarejea na mabo yanakuwa salama lakini ni muhimu pia na tahadhari zikaanza kuchukuliwa mapema ili kujilinda zaidi

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.