SELEMAN Matola,  kocha msaidizi wa Simba amesema kuwa ni suala la kusubiri tu kwa sasa kabla ya wachezaji wazembe muda wao wa kuumbuka ndani ya uwanja kufika.

Ligi Kuu Tanzania Bara ilisimamishwa Machi 17 na Serikali kupitia kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kutokana na janga la Virusi vya Corona inatarajiwa kurejea mwezi Juni iwapo hali itakuwa shwari.

Akizungumza na Saleh Jembe, Matola amesema kuwa wapo wachezaji ambao wanazembea program ambazo wamepewa na benchi la ufundi jambo lisilopendeza hivyo muda wao wa kuumbuka unakuja pale ligi itakapoanza.

"Mchezaji anayejitambua na anapenda kazi yake hawezi kukubali awe anasimamiwa kila wakati ila kwa wale ambao bado wanapuuzia muda wao unakuja kwani ligi ikirejea watajulikana tu kwa matendo hivyo wao wenyewe wataumbuka.

"Ningependa kuwashauri kwamba wanapaswa wazingatie kanuni na utaratibu ambao wamepewa na benchi la ufundi kwani mchezo wa mpira huwezi kudanganya bali ni mchezo wa wazi washtuke na kuendelea kuchukua tahadhari kwani Virusi vya Corona vipo," amesema.

Simba ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 71 baada ya kucheza mechi 28

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.