DAVID Molinga, mtupiaji namba moja ndani ya Yanga alikuwa na mpango wa kusepa Bongo kabla ya Machi 18 baada ya Ligi Kuu Bara kusimamishwa Machi 17 na Serikali.
Molinga aliomba ruhusa kwa uongozi ili asepe zake na kuibukia Ufaransa kwa ajili ya kuiona familia yake ila janga la Corona lilitibua mipango yote.
"Muda mrefu Molinga alikuwa ameombwa ruhusa ya kuondoka Bongo ili aelekee Ufaransa ila hakuweza kwenda kutokana na hali kubadilika ghafla kwa upande wa maambukizi ya Virusi vya Corona.
"Uongozi ulikuwa unatambua kuhusu ruhusa yake ila walipomuona bado yupo walimuhoji kilichomkwamisha alieleza kuwa ripoti ya maambukizi nchini Ufaransa ilimtisha akaamua abaki Bongo," alieleza mtu wa karibu.
Molinga ametupia mabao nane kati ya 31 yaliyofungwa na timu hiyo iliyo nafasi ya tatu kwenye msimamo na pointi zake 51 kibindoni
Post a Comment