Rekodi ya mechi ambazo timu moja waliokota mabao zaidi ya matatu nyavuni:- Alliance 4-1 Mwadui, Februari 19 Uwanja wa Nyamagana Mwanza.

David Rishard alitupia matatu na Vincent Sameer alipiga msumari wa nne kwa Mwadui Otu Samweli alicheka na nyavu.

Alliance 1-4 Simba, Uwanja wa CCM Kirumba, Januari 19. Beno Kakolanya alitunguliwa bao la nje ya 18 na Israel Patrick dk 28 ngoma ilipinduliwa na Jonas Mkude dk 45 kisha Meddie Kagere, Clatous Chama na Hassan Dilunga alikomelea msumari dk ya 73.

Kagera Sugar 4-1 Mbeya City, Uwanja wa Kaitaba, Erick Kyaryuzi, Yusuph Mhilu,Frank Ikobela na Geoffrey Mwashiuya walipeleka machungu huku lile la Mbeya City likifungwa na Frank Damas ilikuwa ni Novemba 22 .

Simba 4-0 Mbeya City Uwanja wa Uhuru, Novemba 3 kazi ilianza na Meddie Kagere, Clatous Chama, Sharaf Shiboub na Deo Kanda.

Simba 4-0 Lipuli, Uwanja wa Uhuru ilikuwa Desemba 25.
Francis Kahata alianza Meddie Kagere na Hassan Dilunga alifunga mabao mawili.

Lipuli 5-1 Singida United ilikuwa Novemba 6 Uwanja wa Samora.
Daruesh Saliboko alitupia matatu na Paul Nonga alitupia mawili lile la Singida United lilipachikwa kimiani na Jonathan Daka.

Alliance 0-5 Azam FC, Uwanja wa Nyamagana ilikuwa Novemba 26.
Obrey Chirwa alitupia matatu, Shaban Chilunda akatupia mawili.
Simba 8-0 Singida United Uwanja wa Uhuru ngoma ilikuwa Machi 11 siku tatu mbele baada ya Simba kunyooshwa kwa bao moja mbele ya Yanga

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.