DARUESH Saliboko, mshambuliaji wa Lipuli amesema kuwa miongoni mwa washambuliaji ambao hupenda kujifunza mambo mengi kutoka kwake ni pamoja na John Bocco anayekipiga ndani ya Simba.
Saliboko ametupia mabao nane msimu huu kati ya mabao 35 yaliyofungwa na Lipuli iliyo nafasi ya 13 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara.
Akizungumza na Saleh Jembe, Saliboko amesema:"Bocco ni miongoni mwa washambuliaji wazawa ambao ninapenda kujifunza vitu kutoka kwake kutokana na namna anavyofanya kazi kwa juhudi bila kuchoka hivyo kwangu ni mshambuliaji hatari anayepaswa kuchungwa muda wote.
"Anakupa mambo mengi ndani ya uwanja iwe kazi ni kwako kujua unachukua kipi kwa wakati huo, kwanza ni kiongozi pili anajali wengine hivyo ninakubali kazi yake."
Bocco kibindoni ana mabao manne aliyopachika msimu huu ndani ya Simba yenye mabao 63
Post a Comment