IBRAHIM Ajibu, kiungo mshambuliaji wa Simba amesema kuwa amekuwa akisemwa tangu akiwa nyumbani kuwa ni mvivu ila hakasiriki kwani anajua anachokifanya.
Ajibu amesema ameanza kusemwa kuwa ni mvivu tangu ameanza maisha ya soka jambo ambalo halimpasui kichwa kwa sasa kwa kuwa anajua kile anachokifanya.
"Tangu naishi kwetu nimekuwa nikiambiwa kwamba mimi mvivu lakini mimi ninajua ninachokifanya na shabaha yangu ilipo.
"Sikasiriki kuitwa mvivu kwani ni muda mrefu ninaambiwa kuhusu hilo nafanya mazoezi yangu na ninafanya kile ninachoambiwa na makocha na kwa sasa nakaa kwangu bado ninaambiwa ni mvivu" amesema.
Msimu uliopita Ajibu alikipiga ndani ya Yanga kwa sasa yupo zake Simba iliyo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 71 baada ya kucheza mechi 28.
Post a Comment