IFAHAMU MASHINE MPYA YA NKANA FC INAYOTAKA KUTUA YANGA
MUSSA Mohamed, beki anayekipiga ndani ya Klabu ya Nkana FC ambaye amesema kuwa amezungumza na mabosi wa Yanga juu ya kusaini dili la kujiunga na klabu hiyo atakuwa na kazi ya kupambana na vichwa vinne vya kazi.
Kwa nafasi ambayo anaicheza nyota huyo anayetajwa kuwa ni miongoni mwa mabeki mahiri ndani ya Ligi Kuu ya Zambia iwapo akitua Yanga akubali kuonyesha ushindani wa kweli ili kupata namba kikosi cha kwanza.
Kwa sasa kipenzi cha Luc Eymael kwa nafasi ya beki ni Juma Makapu ambaye ana nafsi kubwa ya kuanza kikosi cha kwanza.
Nyota wengine ambao atakula nao sahani moja ni pamoja na Andrew Vincent, 'Dante', Lamine Moro na Kelvin Yondani ambaye ni mkongwe ndani ya ligi
Post a Comment