INAELEZWA kuwa uongozi wa Simba ulikuwa kwenye vita nzito ya kuwania saini ya mshambuliaji wa Asante Kotoko ya Ghana, Yacouba Songné, raia wa Burkina Faso lakini mshambuliaji huyo amepiga chini ofa hiyo na kujiunga na Medeama ya nchi hiyo kwa dau la Sh milioni 344.
Medeama imefanikiwa kumsajili nyota huyo mwenye uwezo mkubwa wa kufunga huku akizipiga chini Orlando Pirates ya Afrika Kusini, Al Hilal ya Sudan, Inter Allies ya Ghana na Simba ya Tanzania.
Simba ilikuwa ikimhitaji mshambuliaji huyo kutokana na mapendekezo ya kocha mkuu wa timu hiyo, Mbelgiji, Sven Vandenbroeck aliyependekeza usajili wa washambuliaji wapya katika kikosi chake kwa lengo la kusaidiana na Mnyarwanda, Meddie Kagere na nahodha John Bocco.
Mwenyekiti wa Asante Kotoko, Dk Kwame Kyei, amekiri kuondoka kwa mshambuliaji huyo kwa dau la dola 150,000 sawa na Sh milioni 344 kutokana na kushindwa kufikia dau hilo.
“Songne ameonda kwenye klabu yetu kama mchezaji huru katika usajili uliokamilika mwezi uliopita, alikuwa ni mchezaji mzuri ambaye bado klabu ilikuwa ikimhitaji lakini tusingeweza kuwa naye kutokana na kutaka tumpe dola 150,000, pesa ambayo klabu haikuwa nayo.
“Kiukweli kwetu ni masikitiko lakini tusingeweza kuwadanganya mashabiki kama ataendelea kuwepo kwetu wakati tumeshindwa kufikia mahitaji yake ambayo alikuwa akiomba yatimiziwe katika mkataba mpya, hasa upande wa dau,” alisema Dk Kyei.
Post a Comment