UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa iwapo Ligi Kuu Bara itarejea hivi karibuni wachezaji wote wana kazi ikiwa ni pamoja na mshambuliaji wao namba moja Obrey Chirwa kutimiza majukumu yao uwanjani.
Chirwa ametupia mabao nane kati ya 37 yaliyofungwa na matajiri hao wa Dar baada ya kucheza mechi 28 na kujikusanyia pointi zao 54 kibindoni.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC, Zaka Zakazi amesema kuwa wachezaji wote wana kazi kubwa ya kufanya ilikufikia malengo.
“Tunaamini kwamba kwa sasa ligi inaweza kurejea hivi karibuni, kikubwa ambacho kinatakiwa kwa wachezaji wetu ni kuongeza juhudi mara mbili zaidi ili kufikia malengo ambayo tumejiwekea.
“Kuanzia washambuliaji, mabeki na makipa wafanye kazi kutimiza majukumu yao kwani ushindani utakuwa mkubwa nasi pia tunahitaji kufanya vizuri,” amesema Zakazi.

Ligi Kuu Tanzania Bara ilisimamishwa Machi 17 na Serikali kutokana na janga la Virusi vya Corona inatarajiwa kurejea Juni Mosi

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.