IKIWA zimepita siku kadhaa baada ya kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima kuvuta jiko la pili ameibuka na kuwataka wachezaji kuendelea kulinda viwango vyao katika kipindi hiki kigumu cha maambukizi ya Virusi vya Corona.
Niyonzima amesema kuwa licha ya kuwa kuna janga la Virusi vya Corona ambalo haliwaweki pamoja kwa muda mrefu ni lazima kila mmoja kufanya mazoezi.
Inaelezwa kuwa Niyonzima alimuoa Casandra Rayan kuwa mke wa pili na ndoa hiyo ya siri ilifanyika Bagamoyo mkoani Pwani na walihudhuria watu wachache akiwemo nahodha msaidizi wa Yanga, Juma Abdul.
Niyonzima amesema:-"Ipo haja ya wachezaji kuendelea kulinda viwango vyao katika kipindi hiki cha janga la Virusi vya Corona licha ya kuwa hatujui ligi itarudi lini kwa kufanya hivyo itakuwa faida kwao."
Ligi ilisimamishwa Machi 17 na Serikali kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona
Post a Comment