INAELEZWA kuwa msimu huu wa 2019/20 utakuwa wa mwisho kwa kiungo mshambuliaji wa Simba Ibrahim Ajibu kukipiga ndani ya Simba.

Ajibu alitua Simba akitokea Yanga kwa kusaini dili la miaka miwili kwa mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara.

Taarifa zinaeleza kuwa baada ya TP Mazembe kumkatia tamaa ya kumpata kuna timu nyingine nje ya nchi ambayo inahitaji kupata saini yake.

"Ajibu hatakuwepo tena msimu ujao ndani ya Simba iwapo dili lake la kucheza nje ya nchi litakamilika, jina la timu inayomhitaji limefichwa kwa kuhofia mpango kuvurugika," ilieleza taarifa hiyo.

Patrick Rweyemamu Meneja Mkuu wa Simba amesema kuwa hajapata taarifa hizo

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.