JUMA Abdul, nahodha msaidizi wa Yanga amesema kuwa wanatambua wanapitia kipindi kigumu cha matokeo ila hilo haliwafanyi wakate tamaa kutafuta ushindi uwanjani.
Yanga imecheza mechi 23 ipo nafasi ya nne kwenye msimamo ikiwa na pointi 44 kesho itaikaribisha Mbao saa 1:00 usiku Uwanja wa Taifa mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Ushindi walioupata juzi wa mabao 2-0 yaliyofungwa na Ditram Nchimbi, Uwanja wa Taifa mbele ya Alliance, Februari 29 ulikata bundi la sare lililokuwa likiwaandama ambapo walipata sare nne mfululizo.
Akizungumza na Saleh Jembe, Abdul amesema kuwa kuna umuhimu kwa timu kutimiza majukumu ndani ya uwanja jambo ambalo linafanyika kila siku, kinachowafanya washindwe kupata matokeo mazuri ni ushindani uliopo.
"Tukiwa ndani ya uwanja tunacheza na tunafuata maelekezo ya mwalimu ila kikubwa kwa sasa kinachotutesa ni ushindani uliopo hakuna kitu kibaya kama kushindwa kupata matokeo lakini sio kwa wepesi bila kupambana.
"Tunachokifanya kwa sasa ni kujifunza kupitia makosa na kuangalia mechi zetu zinazokuja tufanye nini ili tuwe bora, mashabiki wasikate tamaa uwezo tunao waendelee kutupa sapoti," amesema
Post a Comment