MARCEL Kahezamshambuliaji wa Polisi Tanzania amesema kuwa kesho watakuwa na kazi kubwa mbele ya Mwadui FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Kambarage.
Kaheza amekuwa kwenye ubora wake msimu huu chini ya Malale Hamsini ambaye ni Kocha Mkuu wa Polisi Tanzania amehusika kwenye mabao tisa kati ya 27 waliyofunga Polisi Tanzania akifunga mabao matano na pasi nne za mabao.
Akizungumza na Saleh Jembe, Kaheza amesema kuwa wamekuwa wakipewa mbinu nying zinazowafanya wawe bora jambo analoamini litawapa matokeo chanya kwa wapinzani wao.
Post a Comment