HITIMANA Thiery, Kocha Mkuu wa Namungo amesema kuwa bado wana kazi kubwa ya kulinda uwezo wao na kiwango chao kwa sasa kutokana na ushindani wa ligi kuwa mkubwa.
Namungo jana Februari 29 ilishusha kichapo cha mabao 2-1 kwa Lipuli FC kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Samora.
Akizungumza na Saleh Jembe, Thiery amesema: "Bado tuna kazi ngumu kupata matokeo haina maana kwamba ligi imekwisha hapana kuna mech nyingi za kucheza na ushindani ni mkubwa.
"Ligi siyo ushindi wa mechi moja ama mbili ni lazima kuona namna gani mechi zote unapata matokeo ila kwa hatua ambayo nipo nawapongeza wachezaji wangu," amesema.
Namungo FC ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo ikiwa na pointi 46 kibindoni imecheza mechi 24.

Post a Comment