UONGOZI wa Simba umesema kuwa utaanza kuipigia hesabu Yanga baada ya kumalizana na Azam FC kwenye mchezo wao wa Ligi utakaochezwa Machi 4, Uwanja wa Taifa.
Machi 8, Uwanja wa Taifa, Simba itamenyana na Yanga kwenye mchezo wa pili wa mzunguko wa pili ikiwa na kumbukumbu ya kulazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Taifa.
Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandnbroek, amesema kuwa hesabu zake kwanza ni kwa mechi yake ya Azam kisha akimaliza hiyo itafuata dhidi ya Yanga.
"Mpango wa kwanza ni Azam kisha baada ya hapo tutamalizia na Yanga, natambua utakuwa mchezo mgumu ila acha kwanza tumalizane na Azam FC," amesema
Post a Comment