ANAANDIKA Haji Manara,kupitia ukurasa wake wa Instagram Ofisa Habari wa Simba:-Heri neno kavu na utulivu kuliko karamu ya Mfalme na machafuko ‘Bible’.


"Nilikwenda mwenyewe mchana huu klabuni Yanga,bahati mbaya sana sikuwakuta viongozi wa klabu. Wazee niliowakuta nje baada ya kuwaeleza nimekuja kukabidhi pesa za masimango walinisihi sana nisifanye hivyo na wakaniambia yule ni mgeni hapa mjini na hajui tamaduni zetu na kuniomba nisirejeshe hata thumuni.


 Nimefundishwa kuwatii wazee, na ntarejea kwa Wanasimba walionikabidhi pesa zao,busara itawashauri tupeleke hospitali kwa wagonjwa wasiojiweza,ikiwapendeza tutafanya hvyo!


Kwetu nimefundishwa uungwana,kwetu nimepata malezi bora,kwetu wazazi wangu walinijaza na jeuri ya kutokubali kuonewa wala kunyanyaswa. halaf mm sijatoka Mbwinde,,hilo ni Muhimu sana na ndio maana naweza kuwa Msemaji pekee naweza kwenda klabu nyingine tena mchana kweupeeeee

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.