STAA wa zamani wa Barcelona, Rivaldo amefunguka kuwa uwepo wa  mchezaji Antonie Griezmann ndani ya klabu hiyo kumemkumbusha uwepo wa Coutinho.

 Rivaldo amemfananisha Griezmann katika msimu wake wa kwanza ndani ya Barca kama ambavyo ilikuwa kwa Coutinho.

 Griezmann  amekuwa akipambana katika msimu wake huu wa kwanza ndani ya Barca lakini bado inaonekana mambo  hayajamnyokea.

 Rivaldo alisema: “Unajua Griezmann ananikumbusha ule msimu wa kwanza wa Coutinho ndani ya Barca, kwa bingwa wa Kombe la Dunia ambaye tayari anajua soka la Hispania alitakiwa kuonyesha tofauti hasa baada ya Coutinho kutokuwepo,  hakuna Suarez wala Dembele.

“Nafikiri anatakiwa kuonyesha kitu cha tofauti kwani Messi  hana muda mrefu ndani ya klabu hiyo tunaamini yeye ndiyo anapaswa kuiga kila kitu kama mbinu na staili za Barca.

“Barcelona ilimsajili kutokana na ubora wake na yeye anatakiwa kuonyesha utofauti.Hata hivyo Coutinho alitolewa kwa mkopo kwenda kujiunga na Bayern Munich na msimu  ujao anatarajiwa kurejea.

 Griezmann alijiunga Barcelona akitokea Atletico Madrid kwa kiasi cha euro milioni 120, lakini bado hajaonyesha cheche zake ndani ya kikosi hicho.

 Msimu huu katika michuano yote Griezmann amefunga jumla ya mabao 13 tu na kati ya hayo nane amefunga kwenye La Liga

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.