MLINDA mlango wa Mtibwa Sugar, Benedict Tinnoco amesema kuwa miongoni mwa washambuliaji ambao huwa anawahofia wakiwa na mpira ni Ibrahim Ajib.
Tinnoco amesema kuwa amekuwa akiwa na hofu muda mwingi akiona Ajibu yupo na mpira kutokana na hatari aliyonayo kwenye kutengeneza pasi za mwisho pamoja na kuachia mashuti.
Tinnoco amesema:"Binafsi nikiwa uwanjani huwa nakuwa makini na washambuliaji wote pamoja na wachezaji wa timu pinzani, ila Ajibu akiwa na mpira ninamuona ana hatari zaidi kwani anaweza kutengeneza na kufunga.
"Wapo wengine ambao wanafanya vizuri wakiwa na mpira ikiwa ni pamoja na David Molinga, Meddie Kagere wanajua kucheza na lango kwa kuwa wao kazi yao kufunga mimi kazi yangu kuzuia," amesema.
Ajibu anakipiga Simba amepiga jumla ya pasi za mwisho nne na amefunga bao moja ndani ya ligi kwa msimu huu.
Post a Comment