Katika
mchezo wa Jumamosi iliyopita wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba dhidi ya
Yanga, kulikuwa na vita kubwa ya katikati ya uwanja. Mchezo huo
uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini
Dar es Salaam, ulimalizika kwa matokeo ya sare ya mabao 2-2.
Tazama hapa jinsi
ilivyokuwa: SIMBA Clatous Chama Jumla ya pasi ni 40, kuharibu mipango
mara moja, hajapiga pasi ndefu. Shuti lililolenga lango ni moja. Jonas
Mkude Jumla ya pasi 56, kuharibu mipango mara tatu, pasi ndefu tatu,
kupoteza moja.
Mzamiru
Yassin Jumla ya pasi 49, kuharibu mipango mara moja, pasi ndefu tatu ,
kupoteza moja. YANGA Balama Mapinduzi Alimaliza mchezo huo akipiga jumla
ya pasi 36.
Mashuti
alipiga matatu, moja likalenga lango na kuwa bao. Abdulaziz Makame
Alipiga jumla ya pasi 21, akaharibu mipango ya timu pinzani mara tano,
akapoteza pasi saba, akafanikiwa kupiga pasi za mbali mbili. Haruna
Niyonzima Jumla ya pasi ni 53, amepoteza tatu, pasi ndefu mbili,
kuharibu mipango mara tatu.
Post a Comment