Kocha
wa Simba, Mbelgiji Sven Ludwig Vandenbroeck amelalamikia bao la Yanga
akidai kuwa lilifungwa wakati mchezaji wake akipatiwa matibabu nje ya
uwanja.
Alisema
kuwa wakati mchezaji huyo akiomba kuingia uwanjani, mwamuzi hakumuona
na goli likafungwa. Hatahivyo hakutoa lawama kwa mwamuzi Jonesia kwani
alisema dakika zote alikuwa sahihi.
“Siwezi
kumlaumu mwamuzi lakini tulifungwa bao wakati mchezaji wetu akiwa nje
ya uwanja bila mwamuzi kufanya uamuzi wowote, “alisema Vandenbroeck.
Naye
kocha wa Yanga, Boniface Mkwasa alisema mchezo huo ulikuwa mgumu, hasa
pale walipokuwa nyuma kwa mabao mawili, “lakini mchezo ulikuwa mzuri na
wenye ushindani wa hali ya juu. Alisema kuwa walipania kushinda mchezo
huo, lakini walitarajia matokeo hayo.
“Mtokeo tuliyatarajia wachezaji walikuwa vizuri, licha ya kwamba tulitaka matokeo yaushindi katika mchezo huo, “alisema Mkwasa.
Alisema
baadhi ya wachezaji ambao hawakupewa nafasi katika mchezo huo
atawatumia katika mechi zijazo ili kuhakikisha anatengeneza timu bora
zaidi na yenye ushindani katika mbio za kuwania ubingwa.
Post a Comment