Patrick Yondani baba mzazi wa beki kisiki anayekipiga ndani ya Yanga, Kelvin Yondani amesema kuwa mtu atakayemfuata kumjaza maneno ili amwambie mwanae acheze chini ya kiwango mechi ya kesho Jumamosi kati ya Simba na Yanga atamsababishia matatizo ya kupelekwa kituo cha polisi.
Kesho, Januari 4, Simba itamenyana na Yanga kwenye Uwanja wa Taifa ukiwa ni mchezo wao wa kwanza kukutana katika ligi kuu ya msimu huu wa 201920, unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa. Simba wanaingia katika mchezo huu wakiwa vinara wa ligi wenye pointi 34 wakati Yanga wako nafasi ya tatu wakiwa na pointi 24.
Baba Yondani alisema kuwa mtu yeyote atakayejaribu kumfuata na kumwambia amwambie mwanae acheza chini ya kiwango atamsababishia matatizo makubwa ya kupelekwa polisi kwani hatamuacha salama kwa kumshushia kichapo.
“Unajua katika mazingira ya kawaida ninajua mpira na ninapenda mpira, mtu aniambie nimwambie mwanangu acheze chini ya kiwango kisa mechi dhidi ya Simba nitamshushia kichapo kitakachonifanya nipelekwe polisi.
“Sipendi kuona mwanangu anacheza chini ya kiwango kwa sababu najua kazi yake ni bora na ana uzoefu mkubwa kwenye mechi hizi dhidi ya Simba zaidi ya miaka 10, sasa hapo ukijichanganya na kuniambia eti acheze chini ya kiwango lazima nikupige, kikubwa ninaamini mwanangu atafanya kazi kwani anajiamini hata ukimuamsha usingizini yeye ni mwendo wa kazi tu,” alisema baba Yondani.
Miaka ya nyuma pindi timu hizo zilipokuwa zikikutana tuhuma za mchezaji kucheza chini ya kiwango kwa sababu tofauti zilikuwa zikitokea mara kwa mara.
Post a Comment