January 2020


Timu ya soka ya  Simba kuoneshaana ubabe na Costal Union leo ambao mchezo utachezwa  kwenye Uwanja wa Uhuru ukiwa ni mchezo wa ligi kuu.

Simba kwa sasa wako nafasi ya kwanza wakiwa na pointi 44 baada ya kucheza mechi 17, Coastal Union wenyewe wapo nafasi ya tatu na alama zao 30, wamecheza mechi 17 kama wapinzani wao.

Sasa rekodi zinaonyesha kuwa kwa msimu uliopita wa 2018/19 ambao Coastal Union ilipanda daraja, iliambulia kichapo mechi zake zote mbele ya Simba jambo linaloufanya mchezo wa leo kuwa mgumu

KOCHA Mkuu wa Yanga, Luc Eymael amesema kuwa tabia ya kuchezea mpira na chenga za maudhi zinazofanywa na Bernard Morrisson raia wa Ghana, hafurahishwi nayo kwani itaigharimu timu yake.
 Morrison, amecheza mechi mbili sawa na dakika 180, mechi yake ya kwanza ya ligi dhidi ya Singida United timu yake ilishinda mabao 3-1 alionyesha udambwiudambwi wa kuchezea mpira na kutembea juu ya mpira na alifanya hivyo kwenye mechi ya Shirikisho dhidi ya Tanzania Prisons wakati Yanga ikishinda mabao 2-0.
 Eymael amesema kuwa alitumia muda mwingi kuzungumza na Morrison kuhusu tabia yake hiyo na kumweleza wazi anapaswa aiche mara moja kabla haijaigharimu timu.
“Mchezaji mzuri anafanya vitu vizuri uwanjani na kwa vitendo inapofikia hatua anakuwa ni mtu wa kufurahisha mashabiki sio tabia ya nzuri, nilimwambia aache na acheze kwa juhudi kuipa matokeo timu yake hakuna kingine ambacho mashabiki wanahitaji.
“Duniani kote kwa yule ambaye anafuatilia mpira kwa kuzitazama timu kubwa ikiwa ni pamoja na Liverpool, Juventus, Manchester United hakuna anayefanya mambo hayo, kuna Mohamed Salah, Sadio Mane wote wa Liverpool hawafanyi haya mambo ila ni wachezaji wazuri,” alisema Eymael.
Yanga ipo nafasi ya nne kwenye msimamo imecheza jumla ya mechi 15 imejikusanyia pointi 28 na kinara ni Simba mwenye pointi 44 akiwa amecheza mechi 17


UBORA anaoendelea kuuonyesha mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere, katika kupachika mabao umefunika uwezo wa klabu za Singida United na Ndanda FC.

Kagere ndiye kinara wa ufungaji mabao katika Ligi Kuu Bara, ambapo baada ya kufunga bao moja juzi dhidi ya Namungo FC, anakuwa amefikisha mabao 12, idadi ambayo imeshindwa kufikiwa na klabu hizo mbili.

Ndanda wamefunga mabao sita pekee katika michezo 16, waliyocheza ikiwa ni nusu ya yale aliyofunga Kagere, huku wakikusanya pointi tisa, wakifungwa mechi tisa, sare sita na kushinda mchezo mmoja, wakiwa wanaburuza mkia kwenye msimamo.

Wakati kwa upande wa Singida United, wenyewe wamefunga mabao nane katika michezo 17 waliyocheza, wakivuna pointi 10, baada ya kushinda michezo miwili, sare katika michezo minne na kupoteza mechi 11, wakiwa wanashika nafasi ya 19 katika msimamo wa ligi hiyo.

“Siku zote nimekuwa nikipambana kuisaidia timu yangu kupata matokeo, sipendi kushindana na mtu, huwa najitahidi kutimiza malengo yangu," amesema Kagere


KIPA namba moja wa Yanga, Farouk Shikalo Jumatano ya wiki hii aliondoka nchini na kurejea kwao Kenya kwa ajili ya kwenda kutatua matatizo ya kifamilia.

Imeelezwa kuwa staa huyo amekwenda kumuuguza mmoja wa watu wa familia yake ambapo atarejea nchini leo Ijumaa.

Shikalo ambaye alisajiliwa na Yanga akitokea Bandari aliondoka nchini juzi na kukosa mazoezi ya kikosi hicho yaliyofanyika katika Chuo cha Sheria, Ubungo ambapo kwenye mazoezi hayo alikuwepo kipa mmoja tu Metacha Mnata.

Kocha wa Yanga, Mbelgiji Luc Eymael amelieleza Championi Ijumaa, kuwa kipa huyo aliondoka nchini na kurejea kwao Kenya baada ya kuomba ruhusa ya siku tatu kwa ajili ya kwenda kumuuguza mmoja ya watu wa familia yake.

“Shikalo aliomba kuondoka na kwenda kwao kwa ajili ya kumuuguza mmoja ya watu wa familia yake. Lakini ruhusa hiyo ni ya siku tatu na baada ya hapo atarudi tena kwa ajili ya kujiunga na timu kama ilivyo kwa wenzake,” alisema Mbelgiji huyo.


KOCHA Mkuu wa Simba, Mbelgiji, Sven Vanderbroeck anatarajia kuivunja safu yake ya ulinzi inayoundwa na Muivory Coast, Pascal Wawa pamoja na Erasto Nyoni, kisha kuisuka upya.

Vanderbroeck amefikia hatua hiyo kutokana na kutoridhishwa na uwezo wa mabeki hao katika siku za hivi karibuni na zaidi walipocheza dhidi ya Namungo FC, juzi Jumatano. Katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar, Simba ilishinda 3-2.

“Kuna makosa mengi ya kiufundi ambayo yamekuwa yakifanywa na safu yangu ya ulinzi kwa upande wa mabeki wa kati na kujikuta tukifungwa mabao ambayo unaweza kuyaita kuwa ni mepesi.

“Nitafanya mabadiliko na kuna uwezekano katika mechi yetu ijayo dhidi ya Costal Union nikawapana nafasi mabeki wengine,” alisema Vandenbroeck na kuongeza kuwa.

“Katika mechi nne tulizocheza hivi karibuni, licha ya kushinda lakini tumekuwa tukiruhusu mabao.”

Matokeo ya mechi hizo ni: Mbao 1-2 Simba, Alliance 1-4 Simba, Simba 2-1 Mwadui na Simba 3-2 Namungo


THOBIAS Kifaru, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar amesema kuwa mchezo wao wa ligi dhidi ya Yanga hawana presha nao kwa kuwa wamejipanga kuwachapa mapema ili kuzibeba pointi tatu muhimu.

Mtibwa Sugar, jana, Januari,30 ilikuwa Uwanja wa Uhuru ikimenyana na Azam FC, itarejea tena uwanjani, Jumapili, kumenyana na Yanga iliyo chini ya Mbelgiji Lucy Eymael.

Kifaru alisema kuwa wana kazi ngumu ndani ya Bongo ila mawazo yao makubwa ni kushinda mbele ya Yanga mapema ili kupunguza kelele za mjini.

“Unajua timu yetu inatoka kijijini sasa ikishinda kwa hizi timu za mjini inapendeza sana na kuzima zile kelele, tumejipanga na tunatambua kwamba mapema tutashinda na kusepa na pointi tatu.

“Yanga wanaitambua vema Mtibwa, ninaamini wanatambua kwamba watacheza na Mabingwa wa Kombe la Mapinduzi, tuliwafunga Visiwani Zanzibar na kuwarejesha mjini mapema watataka kulipa kisasi kwa hilo wasahau, tunazijua mbinu zao tutawapa tabu,” alisema Kifaru


MWENDO wa Yanga ndani ya Ligi Kuu Bara unashtua kutokana na mzani wake kuwa sawa pande zote mbili kwa upande wa kufunga na kufungwa mabao ndani ya ligi.
Yanga iliyo chini ya Luc Eymael, imefunga jumla ya mabao 15 na imefungwa jumla ya mabao 15 kwenye mechi 15 ilizocheza ambazo ni sawa na dakika 1,350. Yanga ina wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 90 na inafungwa bao moja kila baada ya dakika 90.
Kwenye mabao hayo 15 ambayo wamefunga Yanga, kinara wa kutupia ni David Molinga ambaye ametupia mabao matano, Patrik Sibomana ametupia manne, Mrisho Ngassa ana bao moja na asisti moja,Abdulaziz Makame , Yikpe, Mapinduzi Balama , Mohamed Issa ‘Mo Banka’ na Niyonzima hawa wametupia mojamoja.
Kinara wa kutupia pasi za mwisho ndani ya Yanga kwa sasa ni Deus Kaseke ambaye ana jumla ya pasi tatu alizotoa huku Yanga ikiwa imejikusanyia pointi 28 kibindoni.
Juma Abdul, nahodha msaidizi na beki ndani ya Yanga amesema kuwa wanazidi kupambana ili kuzuia idadi ya mabao ya kufungwa kwani ni kitu ambacho kinamkasirisha Kocha Mkuu, Luc Eymael

MBWANA Samatta, nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania anayekipiga klabu ya Aston Villa amesema kuwa hana cha kuwaambia mashabiki wa Tanzania zaidi ya asante kwa sapoti wanayompa.

Samatta alianza kazi rasmi ndani ya Aston Villa ambayo ilimpa kandarasi ya miaka minne na nusu akitokea Klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji. Mchezo wake wa kwanza ulikuwa ni wa nusu Fainali ya Kombe la Carabao dhidi ya Leicester City na ilishinda mabao 2-1.

Ndani ya dakika 65 alizocheza, Dean Smith, Kocha Mkuu wa Aston Villa alisema kuwa alifanya vizuri na anapaswa kupambana.

Samatta amesema:"Ni kazi ngumu kutafuta maneno ya kuwaambia mashabiki zangu wa Tanzania kwa sapoti ambayo wanaitoa, neno zuri ninaloliona ni kusema asante kwa sapoti, haina kufeli,".

Kesho Samatta atakuwa na kibarua mbele ya Bounemouth ambao utakuwa ni wa kwanza kwake ndani ya Ligi Kuu England.


ACHANA na idadi ya mabao ambayo mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara waliyapata  mbele ya Namungo FC kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Taifa, unaambiwa Simba walikuwa wanawaringishia watani wao Yanga kwamba wamewazidi pointi 16.
Ushindi walioupata kwa mpira wa pasi za uhakika kwa wachezaji wote wa Simba wa mabao 3-2 mbele ya Namungo umetosha kuwafanya wazidi kutamba kwamba wao wanaweza kuwa mbali zaidi ya Yanga kwa kuwa wamejijengea ufalme wa pointi 16 ambazo Yanga wanatakiwa kuzishusha ili kuwashusha.
Udambwiudambwi wa Sharaf Shiboub ulikuwa kivutio kwa mashabiki ambao walianza kumshangaa Ibrahim Ajibu ambaye ameanza kunoga taratibu kuunda mfumo wake ndani ya Simba baada ya kumpa pasi Shomari Kapombe aliyemwanga majaro yaliyokutana na bichwa la Francis Kahata aliyelisindikiza jumla nyavuni hiyo ilikuwa dakika ya 21.
Namungo walitumia dakika 14 kusawazisha bao hilo baada ya safu ya mabeki ya Simba kujichanganya  wote wakiwa ndani ya 18 wakabaki wakiusindikiza kwa macho mpira wa krosi iliyopigwa na Relliants Lusajo ikazamishwa kimiani na Bigirimana Blaise aliyemtungua Beno Kakolanya.
Hassan Dilunga aliwanyanyua mashabiki wa Simba dakika tatu mbele akimalizia pasi ya Meddie Kagere kwa kufunga bao la pili  akiwa nje ya 18 kwa kuachia shuti kali ambalo lilizama moja kwa moja langoni na kumuacha mlinda mlango wa Namungo FC Nurdin Barola akidaka upepo.
Mpaka wanakwenda mapumziko Simba walikuwa wanaongoza kwa idadi ya mabao 2-1 na mashabiki walikuwa hawana habari na mabao hayo bali furaha ya kubaki kileleni na kuwaacha watani zao nyuma kwa pointi 16.
Kipindi cha pili Namungo waliwasha moto na kusawazisha bao kupitia kwa Lusajo aliyeachia mshuti mkali nje ya 18 uliomshinda Kakolanya ila Kagere aliamsha furaha kwa kufunga dakika za lala salama akimalizia pasi ya Shiboub.
Simba imecheza jumla ya mechi 17 kwa sasa kwenye ligi na imejikusanyia jumla ya pointi 44 kibindoni ambazo ni nyingi kuliko za wapinzani wao Yanga wenye pointi 28 walizozipata kwenye mechi 15 walizocheza kwa sasa ndani ya ligi.
Yanga imebakiza mechi mbili mkononi ili kuwa sawa na Simba ila hata wakishinda mechi zote mbili zilizobaki bado mlima wa pointi utabaki kwao wataachwa kwa jumla ya pointi 10 ambazo wanapaswa wazitafute kwa udi na uvumba kuwapoteza wapinzani wao.


TIMU ya Tanzania Prisons ya Mbeya imeamua kukimbia kivuli cha Yanga kilichokuwa inaitesa timu hiyo kwa kushindwa kupata matokeo chanya Uwanja wa Samora waliokuwa wanautimia kwenye mechi zake za karibuni.
Prisons iliyo chini ya Adolf Rishard baada ya kuchapwa na Yanga kenye mchezo wao wa 13 Uwanja wa Samora hawakupata ushindi zaidi ya kuambulia sare kwenye mechi mbili alizocheza hapo akiwa mwenyeji.
Kutokana  na maboresho yanayofanywa uwanja wa Sokoine uliokuwa unatumiwa na Prisons iliwalazimu watafute sehemu ya kuchezea na kuchagua Samora ambapo walikuwa wakipata taabu kushinda kwenye mechi zao zote tatu walizocheza.
Walipoteza kwa kufungwa na Yanga bao 1-0 bao la ushindi Ndanda ya bila kufungana kabla ya kuchapwa mabao 3-2 mbele ya Namungo FC  na kuwafanya wafungwe jumla ya mabao manne na walifunga mabao mawili pekee.
Mchezo wao unaofuata dhidi ya  KMC, Februari Mosi ambao ni wa ligi utachezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma  badala ya Samora, Rishard ameliambia SpotiXtra kuwa uwanja wa mwanzo umekuwa ukimuumiza muda mrefu.

Leo ni siku ya hekaheka kwa wachezaji, mawakala na makocha. Ijumaa ya leo Januari 31 ni mwisho wa dirisha dogo la usajili la majira ya baridi.

Kufikia saa sita ya usiku kwa saa za Ulaya timu nyingi zinatarajiwa kufanya makubaliano ya mwisho na kuuziana wachezaji.

Usajili mkubwa mpaka sasa kwa mwezi huu nchini Uingereza umefanywa na Manchester United jana Alhamisi kwa kumnyakua kiungo Bruno Fernandes kutoka klabu ya Sporting Lisbon.

Kocha wa United Ole Gunnar Solskjaer aliahidi kuwa usajili huo ungekamilika kabla ya leo, na wametoa kitita cha pauni milioni 47. Hata hivyo dau hilo linaweza kuongezeka mpaka kufikia pauni milioni 67.

Mabingwa hao wa Serie A wamekuwa wakimnyatia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 kwa wiki kadhaa sasa na wanaaminika kuwasilisha ombi la kutaka kumsaini siku ya Alhamisi

Robinson alijiunga na Latics kutoka Everton mnamo mwezi Julai 2019 kwa mkataba wa miaka mitatu baada ya kuonyesha mchezo


STAA wa Real Madrid, Eden Hazard, ameanza kufanya mazoezi ya uwanjani baada ya kuwa nje kwa muda mrefu akiuguza majeraha.

Hazard alianza mazoezi hayo juzi Jumanne akiwa na Marco Asensio ambaye naye alikuwa nje kwa muda mrefu kutokana na majeraha.

Nyota hao walikosa mechi kadhaa za timu hiyo ikiwemo kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, Spanish Super Cup na La Liga.

Wachezaji hao walianza mazoezi huku wakiwa wamevaa viatu maalumu vya kuwazuia wasijitoneshe majeraha yao.

Hii ni habari njema kwa kocha wa timu hiyo, Zinedine Zidane hasa kuelekea mechi zao zijazo za Ligi ya Mabingwa Ulaya na La Liga.


Baada ya kuonyesha vitu adimu vilivyomkosha kila Mwanayanga na kuwaumiza wapinzani, straika wa Yanga, Bernard Morrison, ameingia chimbo kutengeneza dawa ya mabeki jeuri.

Morrison aliyetua Yanga katika usajili wa dirisha dogo, amekuwa gumzo kutokana na mbwembwe zake za kuchezea mpira maarufu kama Shobobo.

Katika mechi mbili pekee alizocheza dhidi ya Singida United na Tanzania Prisons, tayari amedhirisha kuwa na kiwango bora, kwani pamoja na kutoa burudani, ameisadia timu yake kupata ushindi.

Sasa kwa taarifa yao wale wanaumizwa na miondoko yake uwanjani, wajiandae kuona vitu vingine vipya na safari hii mabeki wajipange.

Baada ya michezo miwili aliyocheza, Morrison amebaini kuna mabeki wabishi na watamkamia katika mechi zijazo, hivyo ameamua kujifungia ndani kupitia video za michezo yote ya timu za Ligi Kuu Tanzania Bara.

Morrison ameeleza kuwa kwa kipindi walichopewa mapumziko, anakuwa bize kuangalia video za mechi mbalimbali za Ligi Kuu Bara ili kubaini aina ya uchezaji wa mabeki atakaokabiliana nao.

“Nimeona ni vizuri kupitia video za timu nitakazocheza nazo, nipate vitu vitavyonisaidia uwanjani, najua safari hii mabeki watakuwa wamejipanga kukabiliana na mimi,’ alisema winga huyo raia wa Ghana.

Katika mechi mbili alizocheza, nyota huyo wa Yanga amefunga bao moja na kutengeza nafasi za mabao mawili ‘assists’. 


WAKATI nyota wa Yanga raia wa Ghana, Bernard Morrison, akiendelea kuwafanya wapenzi wa timu hiyo washindwe kuamini anachofanya uwanjani, kocha mkuu wa Yanga, Luc Eymael, anatarajia kushusha vifaa vingine zaidi yake.

Moja ya kifaa kingine kilichoshuka jijini kimyakimya ni raia mwingine wa Ghana, Joseph Quansah.

Quansa mwenye umri wa miaka 29 ametokea katika klabu ya Amodaus Professional na tayari ameshamwaga wino kuichezea Yanga miaka miwili.

Taarifa zinasema uwezo wake katika dimba la kati ni balaa kubwa huku naye akiwa na vionjo kama vya mtangulizi wake Morrison.

Morrison amekuwa gumzo jijini kutokana na vitu anavyofanya uwanjani, ambavyo mara nyingi wadau wa soka Tanzania walikuwa wakivishuhudia kupitia runinga wakati wanangalia mechi za nje.

Lakini safari hii, wanajionea wenyewe katika ardhi ya Bongo baada ya mchezaji huyo kusajiliwa kipindi cha dirisha dogo lililofungwa Januari hii na baadaye pacha wake naye anatua Jangwani.

Habari njema kwa Wanayanga wakati wakiendelea kupata burudani ya nyota hao, kocha wao Eymael ameahidi kukamilisha idadi yake kwa kushusha mchezaji mwingine ili kufikisha idadi ya watatu anaowahitaji kikosini.

Eymael ambaye ndiye aliyehusika kumleta nyota huyo, alisema anajua sehemu atakayowatoa wachezaji hao na alishindwa kuwasajili dirisha dogo baada ya kuchelewa kutua nchini.

“Morrison ni mchezaji mzuri, ila anahitaji wasaidizi katika kuimarisha safu yangu ya ushambualijia ili kufunga mabao mengi, nisingechelewa kuja ningesajili wachezaji wengine watatu kama huyu haraka.

“Hata hivyo bado lengo langu liko pale pale, nitatimiza wachezaji hao ili kuimarisha kikosi changu, nia yetu ni kutwaa ubingwa msimu huu ili kuleta furaha kwa Wana Yanga,” alisema kocha huyo raia wa Ubelgiji.


KLABU ya Yanga kupitia kwa mdhamini wao Kampuni ya GSM leo Januari 30, 2019 wamefanikisha kutoa masaada wa fedha mahitaji ya chakula cha miezi mitatu pamoja na kugharimia matibabu ya Anna Majaliwa.

Yanga imetoa msaada huo kwenye familia ya Anna ambaye anasumbuliwa na tatizo la mwili kukosa fahamu ndani ya miaka mitatu jambo lililompelekea kushindwa kupata choo kwa zaidi ya miezi sita.

Akizungumza Anna amesema kuwa alipatabtatizo hilo kwa zaidi ya miaka hiyo mitatu jambo linalomfanya kupata tabu kila kukicha hivyo anawashukuru sana Yanga kupitia mdhamini wao GSM kwa kutambua tatizo lake.

“Najisiki faraja sana kuiona timu yangu Yanga kupitia kwa mdhamini GSM, ambao kwa namna kubwa wametambua tatizo langu na kujitolea msada huu wa chakula pamoja na godoro ambalo kiukweli sikuwa nalo nasikuwa na uwezo wa kununu,”

“Mbali na hivyo pia nimpongeze sana Naibu Meya wa jiji la Dar es Salaam, Abdallah Mtinika kwa kujitolea kufufua bima yangu ambayo iliisha na nikashindwa kuifufua, ila GSM nawashukuru zaidi kwa kuahidi kushughulikia tatizo langu hadi nitakapopona,” alisema Anna.

Kwa upanda wa Afisa Mhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz, amesema kuwa, mbali na misaada iliyotoleo jana poa GSM itahakikisha inampatia matatibabu Anna hata nje ya nchi huku ikimhudumia chakula kwa muda wa miezi mitatu

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.