JONATHAN Nahimana, mlinda mlango wa KMC ambaye Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroek aliwahi kumsifu kuwa ni mlinda mlango makini ameingia kwenye rada za Azam FC.
Raia huyo wa Burundi ambaye anakipiga pia timu ya Taifa ya Burundi amekuwa kwenye ubora wake msimu huu akichukua mikoba ya nahodha wake Juma Kaseja ambaye alikuwa anasumbuliwa na majeruhi.
Habari zinaeleza kuwa tayari Azam FC imeanza kuonyesha nia ya kuisaka saini ya kipa huyo ili akachukue nafasi ya Razack Abarola ambaye mkataba wake unameguka msimu huu.
Anuar Binde, Ofisa Habari wa KMC amesema kuwa hajapata taarifa hizo kuhusu kipa wao kuhitajika na Azam ila inawezekana ikawa biashara.
"KMC tunaamini kwamba mpira ni biashara, hatujapata ofa yeyote kutoka kwa Azam ila ikiwa ni kweli ni wakati wao kuja mezani na kuzungumza ili kujua nini kitatokea," amesema.
Nahimana aliwahi kukipiga ndani ya Vital'O FC msimu wa 2015.

Post a Comment