UNAI Emery, Kocha Mkuu wa zamani wa Klabu ya Arsenal amesema kuwa hakuwa anahitaji saini ya kinda Nicolas Pepe isipokuwa alikuwa anaitaka saini ya Wilfried Zaha staa wa Crystal Palace.
Emery amesema kuwa alilazimishwa kukubali usajili huo na mabosi zake kwani aliwaambia wazi kuwa Pepe hajakomaa hawezi kutafuta matokeo binafsi ndani ya Uwanja.
Arsenal ilivunja rekodi ya usajili wa Pepe kutoka Lille kwa dau la pauni milioni 72, Agosti mwaka jana lakini amekuwa na uwezo wa kupwa na kujaa ndani ya klabu hiyo.
Unai amesema kuwa dili la Pepe lilivuruga mipango yake kwani alihitaji mtu wa kazi na sio wa kufundishwa kazi jambo lililompa wakati mgumu.
Unai alipigwa chini Novemba baada ya kudumu ndani ya Arsenal kwa muda wa msimu mmoja na nusu na nafasi yake imechukuliwa na Mikel Arteta
Post a Comment