UONGOZI wa Kagera Sugar umesema kuwa umeukumbuka mpira baada ya kuukosa kwa muda mrefu kutokana na janga la Virusi vya Corona.
Machi 17, Serikali ilisimamisha shughuli zote za michezo kutokana na mlipuko wa Virusi vya Corona ambalo ni janga la dunia kwa sasa.
Akizungumza na Saleh Jembe, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema kuwa miongoni mwa vitu ambavyo wamevikumbuka ni mpira ila hawana chaguo kwa kuwa afya ni jambo la msingi.
“Kiukweli kwa sasa tupo ila tumeukumbuka mpira na mashabiki ukizingatia kwamba ni muda mrefu umepita na hakuna ambacho kinaendelea ndani ya uwanja kwa sasa.
“Hatuna chaguo la kufanya kwa sasa kwa kuwa janga lililopo ni kubwa na kikubwa ni kuchukua tahadhari ili kuwa salama,” amesema Maxime.
Kagera Sugar ipo nafasi ya 8 ikiwa na pointi 41 baada ya kucheza mechi 10 kwenye ligi
Post a Comment