PASCAL Wawa, beki kisiki wa Klabu ya Simba amesema kuwa anamuhofia Mungu ambaye ndiye anamuamini katika kila jambo.
Wawa raia wa Ivory Coast anaiongoza safu ya ulinzi ambayo imefungwa mabao 15 kwenye mechi 28  kabla ya ligi kusimamishwa kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona.
Akizungumza na Saleh Jembe, Wawa alisema kuwa kwenye dunia hii anamuhofia Mungu ila akiwa ndani ya uwanja haofii kufanya makosa.
“Mungu pekee ndiye ambaye ninamhofia kwa kuwa anastahili kuheshimiwa lakini nikiwa ndani ya uwanja sihofii kufanya makosa kwani ndiyo mpira wenyewe.
“Ikiwa utakuwa unahofia kufanya makosa hauwezi kuwa bora maana hakuna ambacho utaboresha, ndio maana wakati mwingine nikiwa uwanjani huwa ninajaribu kufunga licha ya kwamba mimi sio mfungaji,” amesema Wawa.

Simba ikiwa imefunga mabao 63 Wawa amehusika kutengeneza pasi moja ya bao kwa kichwa lilifungwa na Meddie Kagere.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.