METACHA Mnata, mlinda mlango namba mbili wa Yanga aliyewakazia washambuliaji wa Simba, Meddie Kagere na John Bocco kuibuka na ushindi kwenye mechi yao iliyochezwa Machi 8, Uwanja wa Taifa amesema kuwa amepewa program maalumu na Kocha Mkuu, Luc Eymael ili kulinda kipaji chake.
Kwenye mchezo huo ambao Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Bernard Morrison, Mnata aliokoa hatari tatu kali langoni mwake na kuwafanya washambuliaji wa Simba watoke mikono mitupu.
Kwa sasa Ligi Kuu Bara imesimamishwa na Serikali ili kuzuia maambukizi ya Virusi vya Corona ambapo wachezaji pia hawatakuwa na mazoezi ya pamoja mpaka hali itakapotulia.
Akizungumza na Saleh Jembe, Mnata amesema kuwa kwa sasa anaendelea kulinda kipaji chake kwa kufanya mazoezi binafsi ambayo amepewa na Kocha Mkuu, Lucy Eymael.
“Kwa sasa hatupo kwenye kambi kila mmoja yupo nyumbani, nina program ambayo nimepewa na Kocha Mkuu (Luc Eymael) ninapambana kulinda kiwango changu na kuchukua tahadhari ya Corona pia.
“Ratiba yangu inaanza asubuhi ambapo ninafanya mazoezi na jioni pia lakini kuna muda ambao ninapumzika sio kila muda ninafanya mazoezi ninapata na muda wa kupumzika pia,” amesema Mnata.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.