LUC Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa anajua ujanja wa wachezaji pale wanapopewa kazi ya kufanya huzembea jambo ambalo atalijua wakati watakapokutana kwenye mazoezi.
Kwa sasa Ligi Kuu Bara imesimama kwa muda kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona ambapo Serikali ilisitisha kwa muda wa siku 30 shughuli zote za mjumuiko.
Eymael ambaye amekiongoza kikosi hicho kwenye mechi 15 kwa sasa yupo zake Ubelgiji akiwa amepewa mapumziko ya muda na mabosi wa Yanga amesema kuwa ameacha programu maalumu kwa wachezaji wake.
"Nimeacha programu kwa wachezaji wangu na ninatambua tabia za wachezaji wa Afrika kwani nimefanya nao kazi ninajua kwamba wapo watakaozembea lakini nitawajua tukikutana kwenye mazoezi.
"Malengo yangu makubwa ni kuona kwamba wanakuwa bora muda wote ndio maana nimewapa programu hiyo endapo wataifuata itawasaidia kuwa bora na tutaendelea kufanya vema kwenye mechi zetu," amesema.
Post a Comment