KOCHA Mkuu wa Lipuli FC, Nzeyimana Mailo amesema kuwa sababu kubwa ya sare ya kufungana mabao 3-3 na Ndanda FC imechangiwa na mlinda mlango wa timu hiyo Deogratius Munish, 'Dida'.

Kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Samora Iringa, Machi 4, Lipuli ilianza kuitungua Ndanda kupitia kwa Paul Nonga aliyefunga mabao mawili ilishindwa kulinda ushindi huo na kulazimisha sare.

 Mailo amesema:'Nimefuatilia mechi nyingi ambazo tumefungwa tatizo nimeona lipo kwa kipa kwani anashindwa kuwa makini na kulinda lango lake, kila timu pinzani inatumia udhaifu wa wapinzani kushinda wao wametumia mlinda mlango kutushinda,".

 Lipuli ipo nafasi ya 12 imecheza mechi 25 ina ointi 29.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.