IMEELEZWA kuwa kuna nafasi kubwa ya nyota wa Yanga Farouk Shikalo kukaa langoni kwa mara ya pili kuokoa micho ya washambuliaji wa Simba wakiongozwa na Meddie Kagere kwenye mchezo wa Jumapili, Machi 8, Uwanja wa Taifa.

Habari kutoka ndani ya Yanga zimeeleza kuwa kwa sasa benchi la ufundi linafanya tathimini ya kupata kikosi makini kitakachoimaliza Simba  kwenye mchezo wao wa pili wa ligi watakapokutana Uwanja wa Taifa.

"Kila kitu kipo sawa na kwa sasa kazi ya benchi la ufundi inafanya tathimini ya mwisho kuona ni nani atacheza, kwa upande wa nafasi ya mlinda mlango huenda akwa Shikalo, ila tusubiri kwa kuwa bado ni mapema," ilieleza taarifa hiyo.

Kagere ametupia jumla ya mabao 15 ni kinara kwa sasa kwenye Ligi Kuu Bara kwenye mechi ya Januari 4,2020 Uwanja wa Taifa alimtungua bao 1 kwa penalti Shikalo.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.