NAHODHA wa timu ya Coastal Union Bakari Nondo amesema kuwa kwenye mchezo wa mpira hakuna suala la kuoneana huruma.

Coastal Union jana iliibamiza bao 1-0 Singida United kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Namfua.

Akizungumza na Saleh Jembe, Nondo amesema kuwa kila mchezaji anaingia uwanjani akiwa na hesabu zake na mpango wao mkubwa ulikuwa kupata pointi tatu.

"Tuliingia uwanjani tukizihitaji pointi tatu jambo ambalo limetokea, suala la kuoneana huruma halipo kwenye maisha ya mpira, kikubwa ni kupambana ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya ligi," amesema.

Coastal Union ipo nafasi ya tano na ina pointi  42, Singida United ipo nafasi ya 20 ikiwa na pointi 12 zote zimecheza mechi 26

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.