BEKI wa klabu ya Valencia, Alessandro Florenzi ametengwa kwa miezi miwili sasa baada ya kukutwa na maambukizi ya aina tofauti.
Beki huyo awali alitengwa peke yake kwa mwezi mmoja baada ya kuugua tetekuwanga(Chikenpox) lakini sasa ametengwa kwa mwezi mmoja baada ya kupata maambukizi ya Virusi vya Corona.
Mchezaji huyo alijiunga na Valencia kwa mkopo Januari mwaka huu akitokea katika klabu ya Roma.
Hivi karibuni alipimwa Virusi vya Corona na akakutwa na virusi lakini alipojipima mwenyewe majibu yameonyesha kuwa hana maambukizi.
Florenzi baada ya kutengwa awali alikosa mechi dhidi ya Atletico Madrid, Atalanata na Real Sociedad, lakini baadaye alicheza dhidi ya Real Betis na alikaa benchi mechi dhidi ya Alaves na Atalanta.
Beki huyo kwa msimu huu amecheza dakika 160 tu kabla ya La Liga kupigwa stop kutokana na mlipuko wa Virusi vya Corona
Post a Comment