UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa tatizo kubwa linaloimaliza timu kwa sasa ni ubutu wa safu yao ya ushambuliaji inayoongozwa na Obrey Chirwa mwenye mabao nane ndani ya Ligi Kuu Bara.
Akizungumza na Saleh Jembe, Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin, amesema kuwa wamekuwa wakiutazama mwenendo wa timu na aina ya matokeo jambo linalowafanya watafute mbinu ya kulimaliza tatizo hilo pale ligi itakapomalizika.
“Kweli tuna tatizo kwenye safu ya ushambuliaji hilo lipowazi lakini kwa sasa hatuwezi kufanya jambo lolote kulimaliza tulichokubaliana ni kwamba tuboreshe mikataba kwanza ya wachezaji tulionao kisha kwenye dirisha la usajili tutaleta washambuliaji ambao watakuwa suluhisho la tatizo letu,” amesema.
Ligi Kuu Bara ikiwa imesimamishwa kwa muda wa mwezi mmoja kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona, safu ya Azam FC imefunga mabao 37 na safu ya mabeki imeruhusu mabao 20 kwenye mechi 28.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.