March 2020


MOHAMED Salah Hamed Mahrous Ghaly ndio jina lake huyu nyota anayekipiga ndani ya Liverpool akiwa ni raia wa Misri na anakipiga pia kwenye timu yake ya Taifa.

Amezaliwa Juni 15,1992 ana miaka 27 ametupia jumla ya mabao 16 msimu huu ndani ya Ligi Kuu England.


Kocha Mkuu wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema kuwa ni miongni mwa wachezaji wanaojituma ndani ya uwanja jambo linalompa nguvu ya kuendelea kupata kile anachokitaka.

"Kufuata maelekezo na kuwa na uhitaji wa kuona anachokitaka kinatokea ni miongoni mwa vitu vinavyomfanya awe hapo alipo," amesema.

Timu yake inaongoza ligi ikiwa nafasi ya kwanza baada ya kucheza mechi 29 na imejikusanyia pointi 82 kibindoni.


SERIE A Ligi Kuu ya Italia kwa sasa imesimama kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona.

Mpaka inasimama vinara wao kwa utupiaji huku Ciro akimkimbiza Cr 7 kwa kumuacha kwa idadi ya mabao sita ipo hivi :- Ciro Immobile anakipiga Lazio iliyo nafasi ya pili na pointi 62 ametupia mabao 27.

C.Ronaldo ametupia mabao 21 ndani ya Juventus ipo nafasi ya kwanza na pointi 63.

Romelu Lukaku anakipiga Inter Milan iliyo nafasi ya tatu na pointi 54 amefunga mabao 17.

João Pedro anakipiga Cagliari timu yake ipo nafasi ya 11 na pointi 32 ametupia mabao 16.

Josip Ilicic anakipiga Atalanta ametupia mabao 15 timu yake ipo nafasi ya nne na pointi 48.


KLABU ya soka ya Azam imempatia programu maalumu ya mazoezi mchezaji wake aliyesajiliwa katika dirisha dogo la mwezi Januari, Khleffin Hamdoun ili kuzoea utamaduni wa Azam FC na kuongeza ujuzi wake baada ya kuonekana kukosa nafasi ndani ya kikosi hicho tangu asajiliwe.
Hamdoun alikamilisha usajili wake kutokea Klabu ya Mlandege Januari 8, mwaka huu na kusaini mkataba wa miaka minne kuitumikia Azam lakini ameonekana kupata wakati mgumu kuzoea mazingira.
Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa Azam Zakaria Thabith ‘zaka za kazi’ amesema kuwa benchi la ufundi limempa programu maalumu mchezaji huyo ambayo itamsaidia kukuza kipaji chake.
“Hamdoun ni kijana mdogo ambaye ana mengi ya kujifunza bado, hivyo kocha amempatia programu maalumu ya kumwezesha kukuza kipaji chake na kumjengea ule utamaduni wa Azam.
“Hii ni kumwandaa ili atakapoingia rasmi kwenye kikosi aweze kufanya yale makubwa ambayo wadau na wapenzi wa Azam wanayasubiri kutoka kwake,” alisema Thabith.

Chanzo:SpotiXtra


DITRAM Nchimbi, mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa kwa sasa anaendelea na programu aliyopewa na Kocha Mkuu Luc Eymael ili kulinda kipaji chake.

Ligi Kuu Bara imesimama kwa muda ili kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona ambavyo vimekuwa janga la dunia kwa sasa.

Mshambuliaji huyo anayeaminika kutumia nguvu nyingi uwanjani kuwasumbua mabeki yupo zake mkoani Songea baada ya ligi kusimama.

Nchimbi mwenye mabao sita ndani ya Ligi Kuu Bara na pasi mbili za mabao amesema kuwa anatambua umuhimu wa kuchukua tahadhari kwa ajili ya kujilinda na Virusi vya Corona pamoja na kuendelea kufuata programu alizopewa na kocha ili kulinda kipaji chake.

 "Nipo vizuri ninaendelea na mazoezi ambayo nimepewa programu na kocha hilo ni muhimu kwani kazi yangu ni mchezaji na ninaendelea na mazoezi," amesema.


UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa ni wakati wa nahodha wa Simba, John Bocco kurejea Azam FC kwa kuwa ndio maskani yake ilipo.

Bocco alijiunga na Simba msimu wa 2017 akitokea Azam FC yenye maskani yake Chamazi.

Ofisa Habari wa Azam FC, Zaka Zakazi amesema kuwa ni wakati sahihi wa nyota huyo kurejea Azam kuendelea na soka.

"Bocco ni mchezaji mzuri na ana uwezo mkubwa akiwa uwanjani kwani anachokifanya kinaonekana, kwa sasa ni wakati wake kurejea Azam FC ili kurejea nyumbani," amesema.

 Msimu huu ndani ya Simba, Bocco amefunga mabao manne na kutoa pasi mbili za mabao.


BERNARD Morrison, kiungo mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa mabao yake yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na dua maalum ambazo zinafanywa na mke wake pamoja na binti yake.

Morrison amesema mkewe anahusika kwenye mabao anayoyafunga kutokana na dua maalum ambazo anazozifanya.

Machi 8 wakati akiifunga Simba, Morrison alikuwepo uwanjani na kushuhudia bao hilo likifungwa.

“Mke wangu na binti yangu wamekuwa wakifnya dua ambazo zinapa nguvu ya kufanya vizuri hivyo shukrani zangu kwao kwa sapoti yao.
  
Morrison amefunga mabao matatu ndani ya Yanga na ametoa pasi tatu za mabao.


HENRIKH Mkhitaryan nyota wa timu ya Arsenal anayekipiga ndani ya Klabu ya Roma kwa mkopo huenda akabaki jumla kikosini humo iwapo watamhitaji.

Nyota huyo mwenye miaka 31 alizaliwa Januari 21,1989 inaonyesha kuwa Kocha Mkuu wa sasa wa Arsenal, Mikel Arteta hana mpango naye.

Mkhitaryan mwenye urefu wa m 1.78 anacheza nafasi ya kiungo mshambuliaji ni nahodha wa timu ya Taifa ya Marekani lakini ana uwezo pia wa kucheza winga wa pembeni. 

Ndani ya Serie A, nyota huyo amecheza mechi 13 na ametupia mabao sita huku akitoa pasi tatu za mabao na amecheza mechi nne za Europa.

JUMA Abdul, nahodha msaidizi wa Yanga amehusika kwenye mabao matano kati ya 31 yaliyofungwa na Yanga kwenye Ligi Kuu Bara.

Abdul ametoa pasi tano ndani ya Yanga na anaongoza kwa kutoa pasi za mwisho.

Beki huyo amesema kuwa sababu kubwa ya kurejea kwenye kiwango chake ni mazoezi na juhudi isiyo ya kawaida. 

"Kikubwa ni mazoezi na juhudi katika kile ambacho ninakifanya kwa kuwa ni kazi yangu na ninaipenda," amesema.

Kwa sasa Ligi Kuu Bara imesimama kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona ambalo ni janga la dunia.

YUSUPH Mhilu, nyota wa timu ya Kagera Sugar amesema kuwa kwa sasa anaendelea na mazoezi ya kulinda kipaji chake ili kuwa bora endapo Ligi Kuu Bara itarejea.

Kwa sasa ligi imesimamishwa kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona ambapo tamko hilo lilitolewa Machi 17 kupitia kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mhilu amesema kuwa anaendelea kufanya mazoezi na kuchukua tahadhari kwa ajili ya kujilinda dhidi ya Virusi vya Corona.

"Bado hali sio shwari kwa sasa dua ni muhimu ili kila kitu kirejee kama zamani na maisha yaendelee kikubwa ni kuona namna gani tunaweza kujilinda na kuchukua tahadhari.

"Kwa sasa bado ninaendelea kufanya mazoezi ili kulinda kipaji changu na kuchukua tahadhari kwa ajili ya kujilinda dhidi ya Virusi vya Corona," amesema.

Mhilu ametupia mabao 11 ndani ya Ligi Kuu Bara na ametoa pia pasi mbili za mabao.


BEKI wa Real Madrid, SERGIO Ramos amesema kuwa anatambua kuwa wanapita kwenye kipindi kigumu kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona.

Ramos, jana Machi 30 alikuwa anatimiza miaka 34 na mashabiki wengi walimtakia kheri ya kumbukizi kwa nyota huyo raia wa Hispania.

 Kupitia ukurasa wa mtandao wa Instagram, Ramos ameandika hivi: “ Asanteni wote kwa kunitakia kheri katika siku yangu ya kuzaliwa ingawa najua kwa sasa tunapitia wakati mgumu, lakini tutaendelea kupambana,”amesema.


NYOTA Erling Braut Haalad anayekipiga Dortmund kuhusu Virusi vya Corona ni lazima tuungane wote katika mapambano.

Virusi vya Corona vimekuwa janga la dunia ambapo kwa sasa shughuli nyingi zimesimama kupisha maambukizi zaidi ya Virusi hivi.

"Hili janga ni letu sote iwapo utajihisi upo peke yako katika kupambana nalo usifikirie hivyo, ni lazima tuungane katika mapambano.

"Tunahitaji utulivu wa akili na fikra kwenye mapambano haya ili tuweze kupita na kushinda salama.

"Nina amini Mungu wetu atatufanyia njia nasi tutatoka kwenye mtihani huu mgumu," amesema.


GADIEL Michael Mbaga alitua Simba kama sahihisho la Mohammed Hussein Zimbwe kwa maana ya kuwa akionekana ni bora kwa mambo kadhaa.

Wakati anatua Simba, Zimbwe amekuwa bora zaidi, kwa sasa ni namba tatu kwa kiwango bora na anafanya vizuri.

Maana yake, Gadiel analazimika kuanza kupigania namba upya licha ya kwamba alikuwa tegemeo Azam FC na Yanga.

Mpira ndio uko hivi, unataka mapambano kila kukicha na lazima uendelee kujituma ili upate namba na ukipata ujitume kubaki nayo.

Hawa wote ni vijana wa kitanzania wanaopambana na maisha na nia yao ni kujijenga na hakuna ubishi wote ni mabeki wazuri lakini katika maisha, mapambano ni muhimu.

Huu ni mfano mzuri wa maisha kwamba mambo mazuri yanapatikana kupitia Juhudi na Maarifa, yanatofuata yanakuwa ni nyongeza.



AINSLEY Cory Maitland-Niles, raia wa Uingereza hana uhakika wa kubaki ndani ya kikosi cha Arsenal kwa sasa.
Mikel Arteta, Kocha Mkuu wa Arsenal amekuwa hana mpango wa kumtumia nyota huyo kwenye mechi zake za hivi karibuni kabla Ligi Kuu England haijasimamishwa kutokana na kupisha janga la Virusi vya Corona.
Kiungo huyo mwaka 2015-16 alikipiga ndani ya Ipswich Town kwa mkopo ana umri wa miaka 22 alizaliwa Agosti 29,1997.
 Nyota huyo anakipiga kwenye timu ya chini ya miaka 23 ndani ya Arsenal ambapo amecheza mechi moja na hajafunga bao wala kutoa pasi ya bao.

UONGOZI wa Simba umempa pongezi Francis Kahata kwa kujitolea kwa jamii yake nchini Kenya.

Kahata ambaye kwa sasa yupo nchini Kenya alitoa msaada wa lita 10,000 za maji safi katika eneo la Mathare, jijini Nairobi ikiwa ni kwa ajili ya mapambano ya Virusi vya Corona.  

Ofisa Habari wa Simba Haji Manara amesema kuwa ni jambo la msingi kwa nyota huyo kuisaidia jamii jambo ambalo ni la msingi.


LUIS Gustavo Dias ni kiungo raia wa Brazil anayekipiga ndani ya klabu ya Fenarbahce kwa sasa.

Kwenye maisha yake ya soka ni timu ya Vfl Wolfsburg alicheza mechi nyingi ambazo ni 109.

Ilikuwa ni 2013-2017 na alifunga mabao saba, pia alikipiga Bayern Munich 2011-13 ambapo alifunga mabao sita baada ya kucheza mechi 64.


Kwa sasa akiwa na timu yake ya Fenarbahce amecheza mechi 14 na kufunga mabao mawili wakati kwenye tmu yake ya Taifa amecheza mechi 41 akifunga mabao mawili.


BERNARD Morrison, kiungo mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa kazi kubwa kwa sasa ni kujiweka fiti ilikuwa imara.

Morrison amekuwa kwenye ubora wake licha ya kucheza kwa muda mfupi baada ya kujiunga na Yanga akitokea nchini Ghana tayari amefunga mabao matatu kwenye ligi.

Kwa sasa Ligi Kuu Bara imesimama kwa muda ili kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona.

"Muhimu kwa kila mmoja kuchukua tahadhari na kufanya mazoezi kwa wachezaji kwa sasa tunapitia kipindi kigumu lakini ni lazima tuungane kufanya ibada na kufuata kanuni za afya," .


JACK Grealish, nahodha wa Aston Villa ameomba radhi baada ya kuvunja agizo la Serikali la kujifungia ndani wakati huu wa mlipuko wa virusi vya Corona.

Grealish, anacheza na nyota wa Tanzania Mbwana Samatta, amesema rafiki yake ndiye amemshawishi kufanya kosa hilo.


“Kila mtu kujifungia ndani ni wakati mgumu kwa sasa, nilipata simu kutoka kwa rafiki yangu akitaka nikamuone kwake, na kwa ujinga, nilikubali kufanya hivyo. Sitaki mtu yeyote afanye kosa kama hili, hakika nahitaji kukaa nyumbani na kufuata maagizo yaliyowekwa” amesema.

Ligi Kuu England imesimamishwa kwa sasa kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona inatarajiwa kurejea Aprili 30 iwapo hali itakuwa njema.


MEDDIE Kagere, mshambuliaji wa Simba amesema kuwa anapenda kazi yake ya mpira jambo linalomfanya afurahie kufunga kila wakati akiwa ndani ya uwanja.

Ligi Kuu Bara kwa sasa imesimama ili kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona wakati ligi ikisimama, Kagere alikuwa amefunga mabao 19.

Kagere amesema:"Ninaipenda kazi yangu ndio maana nikiwa ndani ya uwanja ninafunga na ninafurahi pamoja na wachezaji wenzangu.

"Ninatambua kuwa kazi kubwa ya mchezaji ni kutimiza majukumu yake kwa wakati," .

LIONEL Messi nahodha wa Barcelona, amesema kuwa jambo la wachezaji kukatwa mshahara limechelewa kufanyika kwa sababu wachezaji walikuwa wanapambana kuisadia klabu pamoja na kuwasiaidia wale walioathirika.

Hatua hiyo ya kukatwa mshahara huo ni kwa ajili ya kuwachangia wafanyakazi wa Barcelona kulipwa mshahara pamoja nakuwasaidia waathirika wa Virusi vya Corona.

Uongozi wa Barcelona umekubaliana kuwakata wachezaji  asilimia 70 ya mishahara.

Messi,amesema:- "Kwetu wakati umefika, tutakatwa asilimia 70 ya mishahara yetu katika kipindi hiki. Pia tutaisaidia klabu ili wafanyakazi wengine walipwe asilimia 100 ya mishahara yao nadhani suala hili lilichelewa," .

  
AISHI Manula mlinda mlango namba moja wa Simba amesema kuwa Bernard Morrison wa Yanga anastahili pongezi kwa kumtungua bao kwenye mchezo wa watani wa jadi uliochezwa Machi 8, Uwanja wa Taifa.

Morrison alifunga bao la ushindi dakika ya 44 kwa mpira wa adhabu akiwa nje ya 18 lilidumu mpaka mwisho wa kipindi na kuipa pointi tatu Yanga.

 Manula amesema kuwa sheria zote alizofundishwa na makocha namna ya kupanga ukuta alizifuata mwisho wa siku akafungwa

“Kwa goli lile, golikipa unatakiwa kupiga makofi na kumpongeza mpigaji," ,


Chanzo EFM

Mbaraka Yusuph, mshambuliaji wa Azam FC  amesema kuwa kwa sasa anaendelea na mazoezi binafsi akiwa nyumbani ili kurejea kwenye kasi yake ya zamani.

Mbaraka alikuwa nje kwa muda mrefu kutokana na kusumbuliwa na majeraha, amerejea kikosini hakupata nafasi ya kucheza mpaka Ligi Kuu Bara iliposimamishwa kutokana na kuzuia maambukizi ya Virusi ya Corona.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mbaraka amesema kuwa amekuwa akiendelea na mazoezi nyumbani jambo ambalo anaamini litampa nafasi ya kurejea kwenye ubora.

"Ninaendelea na mazoezi binafsi nyumbani nina imani itakuwa na manufaa ya kurudisha kipaji changu kikubwa ni kuomba Mungu hali itulie kwa sasa.

"Changamoto kubwa ambayo tunapitia kwa sasa ni kushindwa kuwa uwanjani kwa pamoja lakini hamna namna ni lazima tujilinde na tufuate kanuni za afya," amesema.

Azam FC ipo nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 54 baada ya kucheza mechi 28.


MSHAMBULIAJI wa KMC, Salim Aiyee amesema kuwa sababu kubwa inayomfanya Meddie Kagere wa Simba kufunga mabao mengi ni muunganiko anaoupata ndani ya Simba pamoja na kutokuwa na majeruhi.

Aiyee alijiunga na KMC akitokea Mwadui FC ambapo alikuwa mshambuliaji tegemeo alitimiza majukumu yake kwa kufunga mabao mawili muhimu kwenye mchezo wa play off dhidi ya Geita na kuifanya timu hiyo kubaki ndani ya Ligi Kuu Bara.

Kwa sasa Aiyee amefunga bao moja timu yake ikiwa imecheza mechi 29 ipo nafasi ya 15 na pointi zake 33 ilikuwa mbele ya Yanga wakati KMC ikishinda bao 1-0.

"Kagere anafunga mabao kutokana na aina ya wachezaji anaocheza nao jambo linalompa nafasi ya kufunga pale anapopata nafasi, pia hajawa na majeraha ya mara kwa mara ndio maana akipata nafasi anafunga," amesema.

Kagere amefunga mabao 19 ndani ya Ligi Kuu Bara akiwa ni kinara wa kutupia.

PAUL Nonga, nahodha wa Lipuli amesema kuwa kinachomfanya kuwa bora ndani ya Lipuli ni kutokana na ubora wa wachezaji anaocheza nao.

Nonga ni miongoni mwa manahodha wazawa wenye mabao mengi ndani ya Ligi Kuu Bara akiwa amefunga mabao 11 nahodha mwingine mwenye mabao sawa na Nonga ni Reliants Lusajo anayekipiga Namungo.

Akizungumza na Saleh Jembe, Nonga amesema kuwa kinachombeba ndani ya Lipuli ni pamoja na ubora wa wachezaji ambao anacheza nao kwa kuelewana na kupeana majukumu.

"Aina ya wachezaji ambao ninacheza nao pamoja na namna ambavyo kila mmoja anapokea majukumu aliyopewa ni vitu muhimu kuzingatia kwani vinaongeza ubora," amesema.


DOGO mpya wa Barcelona, Pedro González López amesema hajui cha kufanya siku atakapokaa pembeni ya staa wa timu hiyo, Lionel Messi, Pique au Suarez kwani itakuwa siku ya kipekee kwake.

 Pedri  anamiaka 17 tu amesajiliwa na Barca akitokea katika timu ya vijana  ya Las Palmas na msimu mpya atakuwa ndani ya timu yake hiyo.

“Ikitokea nimekaa pamoja na Messi, Pique au Suarez ndani ya vyumba vya kubadilishia nguo  sijui kwangu itakuwaje ila naisubiri sana siku hiyo.

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.